Home | The Ministry | Service Charter | Projects | Policies | Publications | News & Events | Speeches | Tenders | FAQ | Links | Contact Us
rss
Subscribe to RSS News
Comments / Maoni

Ministry of Infrastructure Development

Its mission is to facilitate provision of an economic, safe and reliable construction industry, transport and services, meteorology, electrical and mechanical services, government buildings and stores that meet the needs of the public through development and implementation of appropriate sector policies, strategies and standards.

News and Highlights

Ahadi za Kikwete Miundombinu kutekelezwa-Dk Kawambwa

Minister of Infrastructure and Development
Wizara ya Maendeleo ya Miundombinu imesema ahadi alizotoa Rais Jakaya Kikwete kwa nyakati tofauti zikiwamo za wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 ni amri, zote zitatekelezwa.

Waziri wa wizara hiyo, Dk. Shukuru Kawambwa amesema bungeni kuwa serikali imedhamiria kutekeleza ahadi hizo, ukiwamo ujenzi wa barabara kama alivyoahidi Rais.

Kwa mujibu wa Dk. Kawambwa, Serikali ya Awamu ya Nne imejipanga kuhakikisha kuwa ahadi hizo zinatekelezwa sanjari na ahadi za kwenye Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2005.

Dk. Kawambwa alilieleza Bunge kuwa baadhi ya ahadi zimeanza kutekelezwa kulingana na uwezo wa bajeti na kwamba serikali itajitahidi kupata fedha kadri itakavyoweza.

Alisema serikali imeanza kutathmini fursa nyingi za kupata fedha za ujenzi wa miundombinu, ikiwamo mikopo ya muda mrefu na kwamba, fursa hizo zitaainishwa katika sera maalumu.

Aliyasema hayo wakati akijibu hoja za wabunge wakati Bunge lilipokaa kama Kamati ya Matumizi kupitia vifungu vya bajeti ya Wizara hiyo iliyopitishwa Alhamisi saa mbili usiku.

Awali, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, John Cheyo, alisema tatizo si fedha, bali menejimenti ya miradi ya ujenzi wa miundombinu. Alisema fedha zinazopangwa kwa ujenzi wa barabara zinatumika vibaya na gharama zimekuwa zikipanda bila sababu za msingi.

Ministry of Infrastructure Development

Tancot House, Pamba Road / Sokoine Drive, P.O. Box 9144, Dar es Salaam | Phone +255 22213 7650 - 6 | Fax +255 222112751