Home | The Ministry | Service Charter | Projects | Policies | Publications | News & Events | Speeches | Tenders | FAQ | Links | Contact Us
rss
Subscribe to RSS News
Comments / Maoni

Ministry of Infrastructure Development

Its mission is to facilitate provision of an economic, safe and reliable construction industry, transport and services, meteorology, electrical and mechanical services, government buildings and stores that meet the needs of the public through development and implementation of appropriate sector policies, strategies and standards.

News and Highlights

Daraja la Umoja Kukamilika 2009

Purpose: Ujenzi wa daraja kuunganisha Tanzania na Msumbiji
Sub Sector: Miradi ya Maendeleo
Location: Mtambaswala

Ujenzi wa daraja linalounganisha nchi za Tanzaia na Msumbiji ambalo linaendelea kujengwa huko Mtambaswala katika wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara, sasa umeelezwa kukamilika mwezi Novemba 2009.Awali kwa mujibu wa mkataba, Mkandarasi anayetekeleza kazi za ujenzi wa daraja hili M/S China Geo-Engineering Corporation kutoka China alitakiwa kuwa amekamilisha ujenzi huu mwezi Novemba mwaka huu (2008).

Taarifa hii ilitolewa wakati wa kikao cha pamoja kilichowakutanisha Mawaziri wenye dhamana ya ujenzi wa daraja hilo kutoka Tanzania na Msumbiji ambao walikutana mwishoni mwa wiki (19/09/2008) huko Negomane, Msumbiji ili kujadili maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo. Mawaziri waliohudhuria kikao hicho ni Mhe. Fellicio Pedro Zacarias ambaye ni Waziri wa Ujenzi na Nyumba wa Jamhuri ya Msumbiji wakati ambapo kwa upande wa Tanzania, Mhe. Hezekiah Chibulunje (Mb), Naibu wa Waziri wa Miundombinu alihudhuria kwa niaba ya Waziri wa Miundombinu.

Ujenzi wa daraja hili ambalo linajulikana kama ‘Daraja la Umoja’, ni matokeo ya wazo lililotolewa na Marais waasisi wa nchi hizi mbili ambao ni Hayati Julius Kambarage Nyerere wa Tanzania na Hayati Samora Machel wa Msumbiji.


Wazo hili lilijumuishwa rasmi katika Mkataba wa Ushirikiano uliosainiwa mwezi Septemba, 1975.Uzinduzi wa ujenzi wa Daraja la Umoja ulifanyika mwaka 2005 kwa Marais Benjamin William Mkapa wa Tanzania na Rais Armando Emilio Guebuza wa Msumbiji kuweka jiwe la msingi katika eneo hilo la mradi.

Daraja la Umoja ambalo litagharimu kiasi cha shilingi bilioni 30, lina urefu wa mita 720 likiwa na uwezo wa kupitisha magari mawili na sehemu ya watembea kwa miguu kwa wakati mmoja.

Mradi huu pia unajumuisha ujenzi wa barabara ya lami yenye jumla ya urefu wa kilometa 10 kwa kuzigawa kilometa 5 kila upande wa daraja. Jumla ya wafanyakazi 400 wakizalendo wameajiriwa katika mradi huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwakilishi wa Mhandisi Mshauri kutoka Kampuni ya Norconsult, ilielezwa kuwa sababu kubwa ya kuchelewa kukamilika kwa mradi huu kwa mwaka mmoja zaidi, ni matatizo yaliyojitokeza katika usanifu wa daraja hili ambao wakati utekelezaji ulipokuwa ukiendelea ilibainika kuwa kuna vifaa ambavyo viwango vyake vinatofautiana na vile vinavyotolewa na watengenezaji. Vifaa hivyo vinakusudiwa kutumika wakati wa ujenzi wa sehemu ya juu ya daraja ambao unaendelea kwa sasa.Mkataba huu unatekelezwa kwa mtindo wa Design and Build yaani Mkandarasi ndiye anayesanifu na pia kujenga mwenyewe.

Hivyo taratibu za kulishughulikia tatizo hili kimkataba zinafanyika ili kuona hatua za kuchukua na kuhakikisha kuwa muda huo wa ucheleweshaji unapunguzwa. Aidha gharama za ziada zitakazojitokeza zitaangaliwa kwa kuzingatia masharti ya mkataba.Hata hivyo taarifa iliyotolewa na Mawaziri waliohudhuria mkutano huu, iliwataka Makatibu Wakuu kutoka wizara hizo mbili husika pamoja na wataalam ambao pia walihudhuria katika Mkutano huo, kulifanyiakazi suala hili kwa lengo la kuhakikisha kuwa mradi huu unakamilika mwezi Septemba 2009 badala ya Novemba 2009 kama mkandarasi alivyoomba.

Maeneo ambayo yameelezewa kuweza kupunguza muda huo ni pamoja na kuongeza muda wa kazi, kuimarisha vitendea kazi pamoja na wataalam wa usimamizi. Haya yote yazingatiwe bila ya kuathiri ubora wa kazi.

Ministry of Infrastructure Development

Tancot House, Pamba Road / Sokoine Drive, P.O. Box 9144, Dar es Salaam | Phone +255 22213 7650 - 6 | Fax +255 222112751