More Highlights...
- Amb. Herbert Mrango - Deputy Permanent Secretary…
- Ministry of Infrastructure - Budget 2010/2011
- Ziara ya Katibu Mkuu Omari Chambo kutembelea mradi…
- UTEUZI WA MWENYEKITI WA BODI YA CHUO CHA BAHARI…
- BODI MPYA YA TPA
- Floods shut Dar – Dodoma, part of the central…
- Ministry of Infrastructure Development restructured…
- TAARIFA KUHUSU MASUALA YA TRL
- Tanzanian minister highlights China’s contribution…
- EAC Roads Sector Projects
- Ujenzi wa MiundoMbinu na msukosuko wa fedha duniani…
- Kilimanjaro International Airport - KIA
- Daraja la Umoja Kukamilika 2009
- ATCL gets lease to fly again
- Tanzania to use $946m to improve its regional…
Site Search
Reports & Policies
To facilitate provision of an economic, safe and reliable constriction industry, transport and services, meteorology, government buildings...

Ministry of Infrastructure Development
Its mission is to facilitate provision of an economic, safe and reliable construction industry, transport and services, meteorology, electrical and mechanical services, government buildings and stores that meet the needs of the public through development and implementation of appropriate sector policies, strategies and standards.
News and HighlightsTAARIFA KUHUSU MASUALA YA TRLWaziri wa Miundombinu Mhe. Dr. Shukuru J. Kawambwa (Mb), mnamo tarehe 17 Septemba 2009, alikutana na waandishi kutoka vyombo mbali mbali vya Habari ambapo aliweza kufafanua mambo kadhaa yanayohusu uendeshaji wa shirika la reli TRL hasa katika kipindi hiki ambapo kumekuwa na changamoto nyingi kwa upande wa uendeshaji.
1.0 UTANGULIZIUendeshaji wa shughuli za Reli umekuwa ukigubikwa na matatizo mbalimbali yakiwemo ya uchakavu wa njia ya reli, injini na mabehewa ya mizigo na abiria. Yote haya yametokana na kasoro mbalimbali zikiwemo za Kimkataba, menejimenti, uhaba wa mtaji na ukosefu wa fedha. 2.0 UTENDAJI WA SHUGHULI ZA RELI KABLA YA UKODISHAJI Katika kipindi kuanzia mwaka 1978 hadi mwaka 1987 baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki utendaji uliendelea kuwa wa wastani wa tani 921,000 kwa mwaka kwa kuzingatia kwamba Shirika liliendelea kutumia vifaa vilevile vilivyorithiwa kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hata hivyo, kulikuwa na ongezeko la injini za treni aina ya 88xx zilizotolewa kama msaada kutoka Canada. Mwaka 1988 hadi 1998 utendaji uliendelea kuongezeka hadi kufikia wastani wa tani 1,071,000 kwa mwaka baada ya kupokea injini nyingine tisa (9) za aina ya 89xx na nne (4) aina za 65xx zote kutoka Ujerumani. Kati ya mwaka 1997 mpaka 1998 uchukuzi ulishuka hadi kufikia tani 955,000 kwa mwaka kutokana na athari za mvua za ELinino zilizosababisha uharabifu wa njia ya reli. Mwaka 1997, Shirika liliorodheshwa kwa ajili ya zoezi la ubinafishaji. Kufuatia maamuzi haya hakukuwa na uwekezaji wa aina yoyote kama masharti ya ubinafishaji yanavyoelekeza. Hali hiyo ya kutowekeza katika Shirika iliendelea kwa takribani muda wa miaka kumi (10). Kutokana hali hii uchukuzi ulishuka kutoka kiwango cha tani 1,446,000 kilichofikiwa mwaka 2002 hadi kufikia tani 569,000 mwaka 2007. 3.0 UTENDAJI WA SHUGHULI ZA RELI BAADA YA MKODISHAJI KUKABIDHIWA TRL ilianza shughuli za uendeshaji wa reli tarehe 1 Oktoba, 2007. Takriban baada ya mwaka mmoja na nusu tangu Kampuni ya Reli ikabidhiwe jukumu la kutoa huduma za reli, hali ya utendaji kazi imeendelea kutofikia kiwango cha kuridhisha. Hali hii kwa kiasi kikubwa imesababishwa na uwezo mdogo wa kifedha wa TRL na matatizo ya kiuendeshaji. 3.1 HALI HALISI YA VITENDEA KAZI Takwimu zilizonukuliwa na vyombo vya habari kuhusu hali halisi ya injini, mabehewa ya mizigo na abiria hazikuwa sahihi. Hali halisi ya vifaa vilivyorithiwa kutoka TRC mpaka kufikia Agosti, 2009 ni injini 79, mabehewa ya abiria 106 na mabehewa ya mizigo 1,357. Hali ya vifaa hivi katika mwaka huo huo ilionyesha kuwa, injini zilizokuwa nzima ni 56 wakati 23 zilizobaki zikiwa ni mbovu. Mabehewa ya abiria 93 yalikuwa mazima na 13 mabovu. Mabehewa ya mizigo 1,125 yalikuwa mazima na yaliyobaki 232 mabovu. Hadi mwezi Agosti 2009, hali na idadi ya vifaa hivi imepungua sana ambapo jumla ya injini 36 ndio nzima na 43 zikiwa mbovi. Mabehewa ya abiria 66 ndiyo mazima na 40 ni mabovu. Mabehewa ya mizigo 651 mazima na yaliyobaki 706 yakiwa mabovu. 3.2 MAPUNGUFU YA MTAJI Aidha, kumekuwa na mapungufu yaliyojitokeza katika utekelezaji wa Mkataba wa Ukodishaji. Baadhi ya mapungufu hayo ni pamoja na: • Uhaba wa fedha ambazo zingeweza kufanya matenegenezo ya njia ya reli na kukarabati vyombo vya uendeshaji (Rolling Stock). Mtaji uliowekwa na Wanahisa wakati wa ukodishwaji ulikuwa Tshs. bilioni 20 kwa ajili ya kugharamia uendeshaji wa kampuni na kukopa fedha Kiasi cha USD milioni 44 kutoka Shirika la Kimataifa la Fedha la Benki ya Dunia (International Finance Corporation – IFC) kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya reli. Kutokana na hali hiyo, Wanahisa waliamua kujiridhisha kwanza na mahitaji halisi ya kampuni kwa kutengeneza mpango wa biashara wa miaka kumi (10) ambao utaonyesha mapato na matumizi ya kampuni yenye kuleta ufanisi na kutoa huduma bora. Kazi hiyo bado haijakamilika. • Mgogoro wa wafanyakazi kutokana na Menejimenti ya TRL kutotekeleza makubaliano ya kulipa nyongeza ya mishahara ya kima cha chini yaliyofanywa kati yake na TRAWU. Serikali ilichukua hatua ya kulipa nyongeza ya mishahara ya wafanyakazi. Kila mwezi Serikali inachangia jumla ya Tsh. 522.6 milioni. 4.0 UHALALI WA MKATABA WA UKODISHWAJI WA TRC Waraka wa Baraza la Mawaziri Na.29/2006 uliweka utaratibu wa ukodishaji wa huduma za Shirika la Reli Tanzania (TRC) ambao uliruhusu utumike utaratibu wa ubia “Joint Concessional Financing” katika kuendesha na kugharamia Tanzania Railways Ltd kati ya Serikali na RITES ya India. Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) ilianzishwa kati ya RITES na Serikali ya Tanzania kwa umiliki wa hisa asilimia 51 za RITES ya India na asilimia 49 za Serikali ya Tanzania. Kampuni hii ina mkataba wa ukodishaji wa kuendesha huduma zilizokuwa zinatolewa na TRC kwa muda wa miaka 25. Kwa mujibu wa mkataba wa ukodishaji wa shughuli za TRC, Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) ilikabidhiwa rasmi shughuli za uendeshaji wa reli tarehe 1 Oktoba, 2007. 5.0 MATATIZO YA MKATABA Baada ya TRL kukabidhiwa uendeshaji wa biashara ya huduma za reli, baadhi ya mapungufu na matatizo yafuatayo yamejitokeza, kama vile:- (a) Menejimenti ya Kampuni ya Reli Tanzania kutozingatia mkataba wa ukodishaji; na (b) Mgogoro wa wafanyakazi kutokana na Menejimenti ya TRL kutotekeleza makubaliano ya kulipa nyongeza ya mishahara ya kima cha chini yaliyofanywa kati yake na TRAWU. (c) Dosari zilizobainika kwenye Mikataba ya ukodishaji wa Shirika la Reli (Concession Agreement), Mkataba wa Wanahisa (Shareholders Agreement) na Makubaliano yaliyoanzisha Kampuni (Memarts) ya TRL. 6.0 MATATIZO YA HIVI SASA YA RITES KUZUIA MATUMIZI YA VICHWA VYA TRENI NA MABEHEWA Taarifa iliyotolewa na vyombo vya habari kwamba mikataba ya ukodishaji wa mabehewa na injini za treni haikushirikisha Serikali, ni ya kweli kwa kuwa Mkataba huo ni kati ya TRL na RITES. Aidha, Serikali haijaambiwa wala kuombwa ilipe deni hilo la ukodishaji. Lakini, Serikali kutokana na umuhimu wa uchukuzi na usafirishaji wa huduma za reli imeiomba RITES kusitisha mpango wao wa kuondoa injini za treni na mabehewa ya abiria yaliyokodishwa kutoka RITES na badala yake yafanyike mazungumzo kuhusu mpango wa ulipaji wa ada iliyolimbikizwa. 7.0 HATUA ZILIZOCHUKULIWA NA SERIKALI (i) Serikali iliunda Kikosi Kazi ili kuangalia utendaji na uwezo wa TRL wa kulipa nyongeza ya mishahara ya wafanyakazi. (ii) Serikali kuahirisha ada ya ukodishaji (concession fee) kwa kipindi cha mwaka mmoja; (iii) Serikali kuahirisha kutoza ‘performance bond’ kwa kipindi cha mwaka mmoja. (iv) Serikali kupitia RAHCO kukopesha TRL vipuri na vitendea kazi. (v) Majadilidano ya pande mbili kati ya Wanahisa wa Kampuni ya TRL ya kurekebisha vipengele vya mkataba pamoja na kuandaa mpango mpya wa biashara yanaendelea. 8.0 RAI YA SERIKALI KWA WAFANYAKAZI WA RELI Wafanyakazi wa TRL wanatakiwa kuelewa kwamba Serikali kama Mwanahisa iko katika hatua za juu katika majadiliano yanayohusu mkataba huu. Wafanyakazi wanatakiwa kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kufuata taratibu na kanuni za ajira zao bila kujiingiza katika fujo. 9.0 RAI YA SERIKALI KWA WANANCHI Kwa kuzingatia hali ya sasa ya Kampuni ya Reli (TRL) pamoja na mipango ya kurekebisha hali hiyo serikali inaomba wananchi kuwa wavumilivu kwa kuwa hali hiyo ni ya mpito. Serikali inaamini hali hiyo itarekebishwa na kupatiwa ufumbuzi wa kudumu. |
Reports and Publications
- Ministry of Infrastructure - Budget 2010/2011
- Ziara wa Waziri mikoa ya Morogoro na Ruvuma Machi, 2010
- Ziara ya Waziri wa Miundombinu JNIA, Februari 2010
- First Business Roundtable Meeting Transport Infrastructure Constrains: Challenges and Opportunities
- Creating Sustainable Fiscal Space for Infrastructure: The Case of Tanzania
- Ministry of Infrastructure - Budget 2008/2009
