Home | The Ministry | Service Charter | Projects | Policies | Publications | News & Events | Speeches | Tenders | FAQ | Links | Contact Us
rss
Subscribe to RSS News
Comments / Maoni

Ministry of Infrastructure Development

Its mission is to facilitate provision of an economic, safe and reliable construction industry, transport and services, meteorology, electrical and mechanical services, government buildings and stores that meet the needs of the public through development and implementation of appropriate sector policies, strategies and standards.

News and Highlights

Ujenzi wa MiundoMbinu na msukosuko wa fedha duniani ukifuatiliwa na mkutano wa wakuu wa AU

Mkutano wa 12 wa wakuu wa Umoja wa Afrika ulifunguliwa tarehe 1 mwezi Februari huko Adis Ababa, makao makuu ya Umoja wa Afrika. Mkutano huo utafanyika hadi tarehe 3, na kauli mbiu ya mkutano huo ni "ujenzi wa miundo mbinu barani Afrika".

Viongozi, mawaziri wakuu na wajumbe kutoka nchi zaidi ya 50 wanachama wa umoja huo watajadili ujenzi wa miundo mbinu ya mawasiliano barabarani, nishati barani Afrika, na msukosuko wa fedha duanini.

Miundo mbinu barani Afrika bado iko nyuma, hali hii siku zote inazuia maendeleo ya uchumi na jamii barani humo. Hivi sasa Afrika inakabiliwa na changamoto za kuboresha miundo mbinu. Wataalamu waliona kuwa miundo mbinu iliyoko nyuma kila mwaka inapunguza ongezeko la uchumi wa Afrika kwa zaidi ya asilimia moja.

Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni katibu mtendaji wa kamati ya uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa Bw. Abdoulie Janneh tarehe 29 mwezi Januari kwenye ufunguzi wa mkutano wa 14 wa mawaziri wa mambo ya nje wa bodi ya wakurugenzi ya Umoja wa Afrika alisema, miundo mbinu yenye ufanisi na ya kutegemeka katika mawasiliano ya barabara na nishati ni muhimu sana kwa kutimiza utandawazi wa jamii na uchumi barani Afrika.

Sasa barani Afrika watu wanaoweza kutumia umeme wachukua asilimia 40 tu, na baadhi ya nchi za Afrika zilikumbwa na hali ya upungufu na ukosefu wa umeme, hali hii imeathiri vibaya maendeleo ya uchumi. Licha ya hayo, hali iliyoko nyuma ya mawasiliano pia inakwamisha maendeleo ya uchumi.

Kutokana na kuwa hali ya siasa barani Afrika inaelekea kwa utulivu, nchi nyingi za Afrika ziliweka mkazo kwanza katika kustawisha uchumi katika ujenzi wa miundo mbinu. Takwimu zilizotolewa na Benki ya dunia zimeonesha kuwa, katika miaka kumi ijayo, ujenzi wa miundo mbinu barani Afrika utahitaji dola za kimarekani bilioni 250, na sekta za mawasiliano na uchukuzi, umeme, maji, na upashanaji wa habari ni sekta muhimu zinazowekezwa na serikali za nchi mbalimbali barani Afrika. Ili kuvuta kampuni za nchi za nje kushiriki kwenye ujenzi wa miundo mbinu, serikali za nchi mbalimbali za Afrika zinatekeleza sera zenye unafuu katika kodi na kutoa ruzuku za mitaji.

Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Yang Jiechi alipofanya ziara katika nchi nne ikiwemo Uganda alisema, kauli mbiu ya mkutano huo wa wakuu wa Umoja wa Afrika inaonesha kuwa nchi za Afrika zinatilia maanani kuboresha ujenzi wa miundo mbinu. China inapenda kuimarisha zaidi ushirikiano kati yake na Afrika katika sekta ya miundo mbinu, na inapenda kuendelea kuchangia maendeleo ya jamii na uchumi barani Afrika.

Kauli mbiu nyingine ya mkutano huo ni suala la msukosuko wa fedha duniani. Kutokana na kuenea kwa msukosuko huo, athari mbaya iliyosababishwa na msukosuko huo kwa nchi za Afrika ilionekana hatua kwa hatua, na maendeleo endelevu ya Afrika yaliathiriwa vibaya. Msukosuko wa fedha pia utaathiri vibaya juhudi za nchi za Afrika za kupunguza umaskini.

Kabla ya hapo viongozi wa China waliitaka jumuiya ya kimataifa ifuatilie hali ya nchi za Afrika, na kutopunguza msaada maendeleo ya Afrika kutokana na msukosuko wa fedha duniani. China pia ilisisitiza kuwa haitapunguza misaada kwa Afrika, na inapenda kudumisha ushirikiano na nchi za Afrika katika suala la mageuzi ya mfumo wa fedha wa kimataifa.

Ministry of Infrastructure Development

Tancot House, Pamba Road / Sokoine Drive, P.O. Box 9144, Dar es Salaam | Phone +255 22213 7650 - 6 | Fax +255 222112751